Kinachofanya mtu aheshimike duniani kote pale ni pesa, huu ndiyo ukweli mchungu ambao unapaswa kuusikia kila wakati. Mtu mwenye fedha anaheshimika kila mahali wakati mwingine hata watoto wadogo hutambua thamani ya mtu huyo.
Ila ukiwa huna fedha kila mtu hataona thamani yako, dharau nyingi zitakuwa upande wako, hata wale uliowazidi umri watakuona wewe ni takataka tu, na usiyekuwa na maana yeyote ile katika dunia hii.
Usipokuwa na fedha hata uwezo wako wa kujiamini hupungua pia hata watu wengine wanakua hawakuamini. Wenye fedha ndiyo ambao huaminiwa zaidi na watu wanaowazunguka kuliko wale wasiokuwa na fedha.
Kama unataka kuwa mtu mwenye thamani katika jamii yako basi tafuta pesa, ukitafuta pesa na ukiwa nazo hata vikao vyenu vya familia havitafanyika bila uwepo wako. Si vikao tu bali ukimiliki pesa utajijengea thamani na heshima yako kila mahala.
Tafuta pesa uheshimike na uaminiwe na kila mtu.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya
0 Comments