Ipo tafiti kubwa moja ambayo inayoonesha kuwa mara nyingi umaskini huenda kwa mtu yule aliyeamua kukataa tamaa juu ya maisha yake.
Kama ilivyo ada, maskini wote ndiyo wanaongoza kukata tamaa katika ulimwengu huu, wao huona hawana nguvu ya kuendelea kufanya yale yaliyo ya muhimu yenye kuleta mafanikio makubwa maishani mwao.
Maskini huongozwa na lawama ambazo hazina maana yeyote kwenye maisha. Maskini ni watu ambao ni wepesi sana kukataa tamaa hasa pale zinapojitokeza changamoto fulani maishani mwao.
Sasa ukweli ambao napaswa kukukumbusha siku ya leo ni kwamba ili uweze kuwa mtu wa mafanikio ya kimaisha na kifedha kiujumla hutakiwi kuwa ni mtu wa kukataa tamaa, bali yakupasa kuwa mpambaji, kwa sababu wapambanaji ndiyo hula mema ya nchi.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.
0 Comments