BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Tabia ya ubongo usiyoijua.

Tabia pekee ya ubongo wa mwanadamu ambayo hushangaza wengi ni pamoja na kukosa ujasiri wa kujiamini kwenye kile unachokijua.  Ubongo huchanyanyikiwa zaidi na zaidi hasa pale linapojitokeza jambo jipya ambalo mwanzoni lilikuwa halijulikani, hivyo ubongo hutaka kujua pia jambo hilo.

Kwa mfano ubongo kama umeshikilia katika kuamaini kuwa biashara ya vyakula vya nafaka vinalipa zaidi, mtu mwingine akija  kumueleza mtu huyo kuhusu biashara ya nguo za mtumba kuwa ndizo zenye kulipa zaidi basi akili huamisha mawazo yake ya awali na kuhamia kwenye wazo hilo jingine.

Kitendo hicho cha ubongo kuhamahama kutoka kwenye kile ambacho akili ilikuwa inamini na kwenda kwenye jambo jingine, hufanya akili hiyo kukosa msimamo kwenye kuamini katika wazo moja, hivyo akili huishia kutapatapa kama akili ya mfa maji.

Sasa ikiwa lengo ni kufanikiwa kwenye jambo fulani, ipo haja sana kwako kuweza kuituliza akili yako kwenye kuamini zaidi kwenye eneo lako unaloliamini zaidi, hata ukitokea kuna jambo fulani ambalo ni dili zaidi ya kile unachokiamini basi usikurupuke unachotakiwa kufanya ni kuchunguza kwanza jambo hilo kabla hujaamua kuchukua maamuzi ya kufanya jambo hilo.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments