Mchakato wa uchomaji wa chapati kila mmoja wetu nadhani anaujua vyema, kwamba ili iwe chapati kamili ni lazima ipitie hatua mbalimbali ambazo sina haja ya kuzielezea sana hapa.
Chapati hupitia nyakati ngumu sana kwenye uandaaji wake. Kama ilivyo kwenye uchomaji wa chapati, basi hata wewe ili uweze kufanikiwa kwenye eneo fulani ni lazima upitie hatua ambazo ni ngumu kidogo.
Wakati mwingine itakulazima kuacha kuishi kutokana na mazoea uliyozea ili mradi tu ufikie lengo lako.
Wapo baadhi ya wapo baadhi ya watu watakubeza, au wakati mwingine watakukatisha tamaa, yote hiyo ikiwa ni lengo la kukuvunja moyo, sasa ikiwa ndiyo hivyo tambua yote hayo ni mchakato tu.
Kama ulivyo mchakato wa uchomaji chapati, basi hata wewe unatakiwa kuwa mvumilivu katika mchakato wa upatikanaji wa mafanikio yako, huku ukimini wewe ndiye m-beba mafanikio yako, haijaishi watu wengine wanasema nini kuhusu wewe, unachotakiwa kufanya ni kutotoka kwenye lengo lako mpaka uhakikishe limefanikiwa.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.

0 Comments