BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jifunze kuishi leo yako, ya kale si sehemu yako.

Kila mmoja wetu anapaswa kujifunza kuishi uhalisia wa maisha ya leo, nimesema hivyo kwa sababu changamoto kubwa iliyopo kwenye ulimwengu huu wa leo ni kwamba wengi wao huishi maisha yaliyopita.

Kwa mfano unaweza kukuta mtu fulani anashindwa kufanya biashara fulani eti kwa sababu miaka iliyopita alishindwa kufanikiwa kwenye biashara hiyo. Mtu huyu mara nyingi huwa anazongwa na woga huku akimini hawezi kufanikiwa tena kwenye jambo hilo.

Kafanya hivyo yaani kuishi kwenye maisha yako ya zamani ni kujitenga na mafanikio yako. Mambo yaliyotekea nyuma yaliyobeba maumivu makali naomba yabaki kama historia tu, usiayabebe kwenye moyo na akili yako.

Jifunze kuishi leo, ili uweze kutengeneza maisha yako yenye tija. Yaliyopita yasikuchelewesha kufanya mambo mengine makubwa, amini bado unayo nafasi nzuri ya kuweza kufanya vizuri zaidi na zaidi.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments