Dunia hii pamoja na aina zote za makundi ya watu wanaoishi duniani hapa, lakini lipo kundi moja ambalo lenyewe kazi kubwa ni kuwatoa watu kwenye mstari wa mafanikio na kuwafanya watu hao kuwa waoga kwenye suala la uthubutu.
Watu hawa si wengine bali ni wachanganyaji, wao kazi yao kubwa kwenye maisha yako ni kuuchanganya ubongo wako, pia kukujengea woga wa aina fulani ambao ni sumu sana kwenye maisha yako. Watu hawa ukikaa nao wao kila kitu watakutisha tu.
Ukiwaambia unataka kufanya jambo fulani, watakuambia usifanye kwa sababu kuna hasara lukuki ndani yake, kwa sababu na wewe ni muoga unaacha kuamini kwenye kile unachokiamini kisha kwenda kwenye kile wanachokiamini wao.
Tabia hii ya kuamini mawazo ya wachanganyaji hao ni kujiharalilisha umaskini katika maisha, hivyo kama kweli unataka kufanikiwa kwenye eneo fulani basi unapaswa kukaaa mbali na aina hiyo ya watu ambao hawana mchango wala msaada wowote katika maisha yako.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.

0 Comments