Kila siku fanya mabadiliko kidogo tu kwa kile unachokifanya, na kesho fanya mabadiliko kidogo pia. Utajikuta baada ya muda fulani unasogea kwa sababu ya mabadiliko hayo.
Hutaweza kufanya mabadiliko ya mara moja kama unavyotaka, ila ukiendelea kufanya mabadiliko madogo madogo kila siku, mabadiliko hayo yatageuka na kuwa kitu kikubwa sana kwako.
Unatakiwa kuwa king'ang'anizi kwenye ndoto zako na amua kufanya mabadiliko hayo kidogo kidogo kila siku mpaka uweze kufikia mafanikio yako makubwa. Ukiamua inawezekana.
Hakuna mafanikio ya usiku mmoja. Hakuna anayelala maskini na kuamka tajiri. Kila siku pambana kufanya mabadiliko madogo madogo, mabadiliko hayo yatakufanikisha.
JAMBO LA KUFANYA NA KUZINGATIA, Kidogo ni cha leo, ni kikubwa cha kesho. Kila siku fanya mabadiliko yako yatakayo geuza maisha yako na kuwa ya mafanikio makubwa kwako.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.

0 Comments