BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jinsi ya kuitumia siku yako kwa manufaa.

Kila siku inayoanza kwako, ni siku ambayo inakufikia kama box tupu ambalo unatakiwa wewe ulijaze ndani yake hazina za thamani kama ndoto zako, mipango yako na hatua unazochukua kila siku.

Unatakiwa kujiuliza kama siku yako ikiwa kama box tupu kama nilivyokwambia,  ndani yake utajaza nini, utajaza hazina za mafanikio au utajaza vitu visivyo na mafanikio? Uamuzi unabaki kwako wewe ujaze nini.

Kila siku unatakiwa kuamua kujaza box lako tupu, vitu vitakavyokupa mafanikio ya kesho. Jaza box lako, hatua za kuchukua, matumaini, malengo na mambo mengine mengi ya kubadili maisha yako.

Kila siku yako ikiisha, ukifungua box lako, hakikisha liwe ndani yake lina vitu vya thamani kubwa ambavyo vina weza kubadili maisha yako ya leo na hata ya kesho pia. Je, siku yako umeijaza hivyo vitu vya msingi?

JAMBO LA KUZINGATIA NA KUFANYA, jikumbushe siku yako inakuja kama box tupu. Jaza box hilo mawazo chanya, malengo yako, mikakati mizuri, kujiamini, kujitoa na kila kitu kinachotakiwa kwa ajili ya mafanikio.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments