BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Njia sahihi ya kusonga mbele.

 

Wakati mwingine njia sahihi ya kuweza kusonga mbele na pale ulipo ni kwenda taratibu. Hapa unatakiwa kujifanya mjinga, hapa unatakiwa kufunga breki na kuamua kwenda polepole na haraka zote kuweka pembeni.

Kufanya mambo makubwa, kuwa bize muda wote na kwenda haraka sana, hiyo inaweza isikusaidie sana, na pengine inaweza kukuumiza na kukupotezea mwelekeo wa mafanikio yako ya leo na kesho.

Haraka haraka haina baraka, wahenga walisema. Hata kwenye maisha yako kuna wakati unatakiwa uwe mwangalifu na amua kwenda pole pole kama mwendo wa kobe, kasi kubwa inaweza ikakupoteza.

Kuwa na kasi kubwa halafu isiyo na faida, huko ni sawa na kupoteza maisha yako kabisa. Kwa nini uwe na kasi kubwa itakayoharibu kila kitu kwenye maisha yako na ukabaki unaonekana mjinga tu. 

JAMBO LA KUZINGATIA NA KUFANYA, kuwa na mwendo wa pole pole, unapoelekea kwenye ndoto zako. Mwendo wa kasi sana, unaweza usikusaidie kitu na ukakupoteza. Kuwa makini na nenda kwa kasi unayoimudu.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments