Njia sahihi ya wewe kuweza kujifunza mambo mengi ni kusahau kama unajua vitu vingi. Ikiwa kabla hujajifunza kitu ukijifanya unajua, basi huwezi kujifunza kitu, zaidi utaishia kuwa hapo ulipo.
Akili yako ina uwezo wa kufanya kazi pamoja na wewe, kama utasahau kama unajua mambo mengi, na akili yako itafanya kazi kinyume na wewe, kama utajifanya mjuaji yaani wa kujua kila kitu hata kabla hujajifunza.
Acha kujiwekea upofu kwa sababu ya maarifa yako wewe mwenyewe. Fungua akili yako iweze kuona mambo mengi ambayo yakusaidia wewe mbele ya safari. Kama usipoifungua akili yako, huwezi kujifunza.
Uamuzi ni wako, kuendelea kuifungua akili yako na kujifunza mambo mengi au kujifanya unajua na ukaifungia akili yako. Sumu ya wewe kujifunza, jifanye unajua, basi, hapo umekwisha, hutajua mambo mengi sana.
JAMBO LA KUFANYA KUZINGATIA NA KUFANYA, sahau kila kitu unachojua, anza upya kujifunza, na utajifunza mambo mengi sana ambayo hata hukuwahi kuwaza kama utajifunza mambo hayo.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.

0 Comments