Kufanya kazi kwa bidiii ndiyo wimbo pekee ambao huimbwa na watu wengi, wengi watakwambia ukitaka kufanikiwa katika jambo fulani basi hakikisha unafanya kazi kwa bidii.
Pamoja na uwepo wa wimbo huo nami naomba nikuongezee kiitikikio katika wimbo huo ili uwe wimbo wenye ujumbe wa maana hasa pale unaposikiliza.
Kiitikio cha wimbo huo kinasema "Ogapa kufanya kazi kwa bidii kama kile unachokifanya hakikuongezei fedha maishani mwako".
Ukiendelea kufanya kazi kwa bidiii, huku kile unachokifanya kikiwa hakikuongezei fedha yeyote, kufanya kazi kwa bidii kutakuwa hakuna maana yeyote bali ni sawa na kupoteza muda tu.
Kumbuka; ongezeko la ufanyaji wako wa kazi ni lazima likuongeze fedha pia.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.

0 Comments