Mara nyingi watu wengi hupoteza fedha zao bure kwa sababu ya kufuata mkumbo wa matumizi ya kifedha kutoka kwa wetu wengine huku tabia hiyo ikiwapelekea watu hao kuwa na umaskini wa kudumu maisha yao yote.
Wapo baadhi ya watu, wao kazi yao kubwa huwa ni kuwatazama watu wengine kwenye kila wanachokifanya, hususani kwenye vitu wanavyomiliki na wao kuiga pasina kuangalia umuhimu wa kitu hicho.
Kitendo hicho, huwapelea watu hao kupoteza fedha zao bure hii yote ni kwa sababu waliiga mkumbo wa matumizi ya kifedha.
Ndugu, ikiwa unataka kufanikiwa kifedha basi yakupasa kuacha mara moja tabia ya kuiga matumizi ya fedha kutoka kwa watu wengine. Jifunze kuishi wewe kama wewe, kulingana na kipato chako.
Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.

0 Comments