Unapokuwa umejiwekea malengo yako, acha kuwaza tu matokeo ya mwisho utakayopata, waza juu ya mchakato utakaokufikisha kwenye malengo yako.
Unatakiwa uelewe mchakato wa kuelekea kwenye malengo yako ni kama gari la kukufikisha kwenye malengo hayo. Unatakiwa kuufata mchakato kila siku, hadi ufanikiwe.
Unatakiwa kujua ili mchakato ukamilike, lazima uwe na juhudi na nidhamu. Hayo ni mambo mawili ya msingi ambayo yapo kwenye mchakato wa ndoto zako ulizonazo.
Wengi
wanachukia mchakato, badala ya kuufurahia. Jifunze kufurahia mchakato na habari
ya matokeo yatakuwaje haikuhusu sana, wewe komaa na mchakato, matokeo yatakuja
yenyewe.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.
0 Comments