BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Usifanye kitu kwa kujaribu kwani hautafanikiwa.

Ili uweze kufanikiwa zaidi kwenye kila unachokifanya unatakiwa kujitoa muhanga katika kukifanya kitu hicho. Unapojitoa muhanga katika kutekeleza jambo fulani ni kwamba utaweza kufanikiwa zaidi kwenye kitu hicho kwa sababu haijalishi ni chanagamoto gani ambazo zitajitokeza katika jambo hilo ni kwamba wewe hutokata tamaa bali utaendelea kupambana mpaka tone la mwisho.

Pia unapojitoa muhanga ni kwamba kila kwenye kila ratiba ambayo umepanga kufanya jambo fulani basi haijalishi ni jambo gani litajitokeza ni kwamba utakamilisha kwanza lile ulilokuwa umepanga kisha kwenda kufanya jambo jingine hilo ambalo litakuwa limejitokeza.

Unapoamua kujitoa muhanga katika kutenda jambo fulani ni kwamba utalitenda jambo hilo katika viwango vinavyostahili. Ni muhimu kujitoa kikamilifu kwa sababu watu wengi huwa hawajitoi kikamilifu katika kukamilisha yale wanayotaka yawakamilishie ndoto zao, mwisho wa siku watu hao huanguka anguo ambalo huwapeleka moja kwa moja katika bwawa la umaskini.

Ni muhimu sana kuanzia sasa kwamba kama umeamua kufanya jambo fulani basi ni vyema ukahakikisha kwamba akili, nguvu na moyo wako wote unajitoa kikamilifu katika kutekeleza jambo hilo. Usifanye kitu kwa kujaribu kwani hautafanikiwa, ila kama utafanya jambo kwa kujioa muhanga ni kwamba utafanikiwa vizuri katika jambo hilo.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments