BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Epuka kukataa tamaa maishani.

Watu wengi ni maskini kwa sababu ya ukataji wao tamaa hasa pale  wanapokutana na changamoto fulani kwenye mambo wayafanyayo.

Wengi wetu tumeacha kufanya mambo ya muhimu kwa sababu tulikutana na changamoto ya aina fulani kwenye jambo fulani.

Kitendo hiki cha ukataji wa tamaa ndicho kilichotupa aina ya maisha tunayoishi hivi sasa.

Ila ukweli ambao ni lazima tuambizane kama tutaendelea na tabia hii ya kuacha kufanya mambo fulani ya msingi eti kwa sababu ya changamoto tunazokutana nazo ni ukweli ulio wazi kwamba mafanikio kwetu tutayasikia kwa watu wengine.

Tujitahidi kadri ya uwezo wetu kutafuta majibu sahihi ya kila changamoto tunazokutana nazo na si kukataa tamaa, kwani tukiendelea kukata tamaa hakuna kitu cha maana tukachokifanya maishani.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments