BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hivi ndiyo maisha ya mafanikio yanavyopimwa.

Maisha ya mafanikio hayapimwi kwa wingi kwa idadi ya chrismasi ulizokula, wala maisha ya mafanikio hayapimwi kwa miaka uliyoikumbatia viganjani mwako.

Bali maisha ya mafanikio hupimwa kwa kutazama yale ambayo umeyatimiza  hususani suala la makusudio ya kuumbwa kwako katika sayari hii ya dunia. 

Kwa kutazama yale uliyokwisha kuyatimiza basi  katika mambo hayo, yakupasa uache alama mara baada ya kufa, watu waliobaki basi wakumbuke kwamba ulifanya nini enzi za uhai wako. 

Kumbuka, Uwezo mkubwa ambao mwenyezi Mungu amekuumba nao usiuache uende zake bure bali unapaswa kuufanyia kazi, kazi ambayo itakupa mafanikio yako.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments