Kwenye maisha haya ya kila siku ili uweze kupata ushindi na matokeo chanya kwenye kila jambo unalolifanya au unalotaka kulifanya unapaswa kuiondoa dhana ya woga uliyonayo. Ukiweza kuiondoa dhana ya woga uliyonayo ni lazima utafanikiwa tu.
Ukiwa darasani ili uweze kufanikiwa vyema katika masomo yako hatimaye kufaulu vizuri, ni lazima pia uondokane na woga ambao mara nyingi huwa unajenga ndani mwako ambao huwa unakuzuia kufanikiwa.
Si darasani tu, bali kwenye kila eneo ambalo unataka kufanikiwa, ili eneo hilo uweze kufanikiwa zaidi na zaidi basi unapaswa kuondokana na woga ambao si mpango mzuri kwenye kuhakikisha unapata matokeo sahihi yenye mlengo wa kukupa mafanikio.
Kama tujuavyo kuwa kisaikolojia mwanadamu huongozwa na hisia mbili, ambazo hisia za furaha na hisia za woga katika hili basi unapaswa kutoruhusu hisia za woga zikutawale maisha mwako, kwani ukiziruhusu zikutawale ni lazima utasgindwa kufikia malengo yako.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.
0 Comments