Na ili uweze kufanikiwa katika hili unatakiwa kutenga kiwango kadhaa ya kila pato lako kuwa ni lako, hii ni kwa sababu changamoto kubwa zinazowakumba watu wengi kwenye kila pato wanalolipata huwa hawakumbuki kutenga pato hilo.
Pato hilo unalolitenga unapaswa kuliweka kwa ajili ya akiba, akiba ambayo itakusaidia kwa hapo baadae katika kutimiza majukumu mengine ambayo yatakuwa yanakukabiri.
Jambo hili la kujilipa asilimia kadhaa kwenye kila pato utakalokuwa unalipata unapaswa kulitenga awali kabisa kabla hujatumia pesa hiyo uliyoipata kwenye matumizi mengine.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.
0 Comments