BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Usifanye kazi kwa kutumia nguvu, fanya kazi kwa kutumia akili.

 


Tunaishi katika ulimwengu ambao ulituaminisha ya kwamba " hardwork pays" hii ikiwa na ya kwamba kufanya kazi kwa juhudi kunalipa. Kweli wengi wamepata matokeo makubwa kutokana na kauli hiyo.

Wengi wetu tumekuwa tukitumia juhudi kubwa sana kuweza kufanya kazi zetu ila matokeo tuyoyapata mara nyingi yamekuwa hayaendani na kile tunachokifanya, na kwenye hili ni watu wachache sana ambao huneemeka na utumiaji wa juhudi kwenye yale wayafanyayo.

Inawezekana hata wewe umekuwa ukifanya kazi kwa juhudi kubwa muda mrefu ila kila ukijitazama unaona fika hakuna kitu cha tofauti unachokipata, kila wakati umekuwa ukipata matokeo yale yale miaka nenda  miaka rudi.

Kama wewe ni miongoni mwa watu hao  leo naomba nikuongeze ufahamu kidogo, kwamba kufanya kazi kwa juhudi pekee haitoshi bali ili upate matokeo tofauti na yale uliyoyazoea kayapata unatakiwa kufanya kazi kwa kutumia akili.

Kila wakati waza namna utakavyokuwa bora zaidi ya jana. Kila wakati fanya kazi itakayokusaidia kupata matokeo tofauti na yale uliyoyazoea kuyapata kila siku.

Ili uweze kupata matokeo ambayo umezoea kuyapata basi isome kanuni hii 20/80 Principle Rule. Kwa mujibu wa kanuni hii inayoanzishwa na Paleto inayoitwa Paleto Principle kanuni ya 20/80 ( 20/80 principle).

Kanuni hii inasema  kuwa "asilimia 20 ya nguvu na jitihada zako ni lazima ilete matokeo ya asilimia 80 ya kile ukifanyacho." Rudia tena kusoma kanuni hiyo ili uielewe vizuri.

Kwa mfano kama kama unalima kilimo fulani basi asilimia 20 ya nguvu zako ulizoziwekeza kwenye kilimo hicho ni lazima ilete matokeo ya asilimia 80.

Kanuni hiyo ndiyo ambayo tunaita kutumia akili. Ila changamoto ni kwamba wengi wetu huwa tunatumia asilimia 80 kama uwekezaji kwenye jambo fulani kitu ambacho hutupelekea tupate matokeo kwa  asilimia 20 pekee.

Kitendo cha kuwekeza asilimia 80 ya juhudi zako hatimaye kupata matokeo ya asilimia 20 pekee siyo sawa, ni sawa na kuzima moto wa msitu kwa kupiga chafya, maana yake hakuna mabadiliko ambayo utakuwa unayaona na kuyapata 

Wengi wetu tunapata matokeo ya kawaida kwa sababu tuwekeza nguvu ngingi kwenye kufanya kazi ila tunapata matokeo kidogo, Ukiendelea na kitendo hicho kuwekeza asilimia 80/20 badala asilimia 20 /80  ambayo nimekueleza hapo basi utaendelea kutapata matokeo yaleyale kila siku.

Sasa ikiwa unataka kupata matokeo tofauti yenye kukuletea  mafanikio zaidi kwako tumia kanuni hiyo ya kuwekeza akili zaidi  kuliko kutumia nguvu ambazo zimekuwa zikikukupa matokeo yale yale kila siku.

Mwisho ili uweze kutumia akili itakayokusaidia kupata matokeo tofauti fanya mambo haya kadhaa; 

1. Tumia muda kwenye kujifunza vitu vitakavyokusaidia kuwa bora zaidi, kwa mfano kama unataka kujifunza kujua kingereza basi tafuta sehemu au watu watakaokusaidia kujua kingereza hicho.

2.Lifahamu jambo vizuri kabla hujaamua kuwekeza kwenye jambo hilo. Unaposikia kutoka kwa watu wengine kwamba jambo hili linalipa usikurupuke na wewe kwenda kuwekeza kwenye jambo hilo bali hakikisha unalielewa jambo hilo vyema kabla ya kuamua kujitupa mzima mzima kwenye jambo hilo.

3. Epuka sana kuwekeza kwenye kitu usichokijua kwani huko utapoteza muda na pesa pia. Wengi wamepoteza muda na pesa zao kwa sababu ya kukurupuka kwao kwenye kuwekeza kwenye vitu wasivyovijua kwa undani zaidi, naomba usiwe mmoja wao bali hakikisha unalijua jambo vizuri.

Mpaka nukta hiyo sina la ziada nikutakie siku njema na tafakari njema katika somo letu hilo. Endelea kutumia Mafanikio App kila wakati.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments