Watu wengi tunaishi maisha ambayo siyo yetu, wengi tunapenda kuishi ili kuwaridhisha watu wengine tunaishi maisha ambayo siyo halisi bali tunaishi maisha feki ambayo tumekuwa tukiwaiga watu wengine.
Kuishi huku kunatufanya tuwe ni watu wenye maisha magumu sana. Leo hii unataka uonekane una maisha ya juu, ili jamii ikuone jinsi ambavyo umefanikiwa wakati huo huo hicho unachokiishi siyo ukweli wako.
Leo hii unataka kuwaonesha watu kuwa una maisha ya hali juu kwa kunywa sana vilevi, wakati huo maisha yako ya rohoni unajua kabisa hayo maisha unafeki. Ndugu maisha hayataki mbwembwe, jifunze kuishi maisha yako halisi.
Ukipata pesa ishi maisha ya kawaida, usichachawe ili kuwaonesha wengine kuwa wewe ni nani kwenye suala la kufanya matumizi kila upatapo pesa. Ifundishe akili yako iwe na utulivu wa akili pale ipatapo pesa.
Ishi kulingana na hali halisi ya maisha yako, usiishi ili kuwafurahisha watu wengine, jifunze kuishi kana kwamba hakuna mtu anayekutazama. Fanya kila jamba kulingana na uwezo wako, ukifanya hiki utaishi maisha mazuri kwa sababu hakuna mtu ambaye atakushangaa.
Kila wakati ogopa sana kuishi maisha ya uongo kutokana na mkumbo wa watu wengine, ukifanya hivyo utakuwa unajichimbia kaburi lako kwa mikono yako, maana ake utajitengenezea umaskini kwa mikono yako mwenyewe.
Mtu fulani ikiishi maisha fulani isiige, kwa sababu hujui chanzo chake cha mapato ila kwa kuwa wewe ndiyo unajijua vyema, unajua chanzo cha kipato chako basi ishi maisha yako halisi, narudie usige maisha ya mtu bali ishi maisha yako.
Wako katika maandishi Benson chonya
.png)
0 Comments