Ukisema usubiri uzeeke ndipo uanze kufanya uwekezaji hapo utakuwa unajidanganya mwenyewe! Hiyo itakuwa na sawa na wale wasemao kuwa utakuwa unakumbuka kuwa hukujifunika usiku wakati kukiwa kumeshakucha na ili hali muda wa kuamuka utakuwa umeshafika.
Narudia tena kwamba kama unataka kuishi maisha ya maana hapo baadae muda sahihi wa wewe kufanya uwekezaji ni sasa ukiwa ungali bado ni kijana mwenye nguvu. Kaa chini na tafakari juu ya jambo hili kisha chukua hatua stahiki.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya
.png)
0 Comments