Ili uweze kuwa mtu mwenye thamani kubwa katka dunia hii ni lazima ujifunze kuwa bora kila wakati. Na ili uwe bora ni lazima uwekeze muda wako mwingi kwenye kujifunza zaidi na zaidi.
Kwenye kujifunza ndiko kutakokusaidia sana uwe mtu wa thamani katika sayari hii ya dunia. Kama unataka kuwa bora zaidi kwenye masuala ya kifedha basi unatakiwa kujifunza zaidi mambo yanayohusiana na masuala ya fedha.
Usiwe mvivu hasa pale linapokuja suala la kujifunza, jifunze bila kuchoka kwani kwenye kujifunza kuna mambo mengi sana yatakayokusaidia kuweza kuwa bora zaidi maishani mwako.
Wekeza kwenye kujifunza ili uweze kuwa bora na mtu mwenye thamani kubwa katika dunia hii. Jifunze zaidi, jifunze kila wakati, jifunze bila kuchoka, utafanikiwa.
Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.
.png)
0 Comments