BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Utofauti wa nia na matamanio kwenye kuyasaka mafanikio ya kifedha.

Changamoto kubwa iliyopo kwenye kizazi hiki cha leo wengi watu hushindwa kutofautosha kati ya nia na matamanio. Wengi hudhani matamanio ndiyo nia, hapana hivyo ni vitu viwili tofauti. Ila ukweli usiojua ni kwamba wenye nia ndiyo wananyakua zaidi mafanikio kuliko wale wenye matamanio. Wale wenye matamanio huishia tu kutamani vile wanavyovitaka pasipo kuchukua hatua.

Kwa nukta hiyo nikukumbushe kuwa ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote lile ni lazima uwe na nia juu ya kile unachotaka kufanikiwa. Kila siku nia ndiyo huchukua nafasi kubwa katika kutengeneza mafanikio yako. Ukifanikiwa kuweka nia yako mbele ni lazima ukate shauri kwamba ni lazima kitu unachokitaka kitafanikiwa tu.

Punguza kuwa ni mtu wa matamanio, hatakusaidia kitu, kuwa mtu mwenye shauku na nia juu ya jambo fulani. Kwa mfano kama nia yako ya ndani inakuambia kuwa mwaka huu ni lazima utengeneza milioni hamsini za kwako, jambo hilo linawezekana kweli kama utakuwa na nia ya dhati katika kufanikisha jambo hilo.

Ila kama unaongozwa na matamanio, utaishia tu kutamani hizo milioni hamsini, na hakuna utakachoweza kufanikisha kwa sababu hauna nia juu ga jambo hilo bali wewe una matamanio tu. 

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments