Na kama ikitokea umefariki, je familia yako itaishi maisha mazuri, au ndiyo wataanza kugombania mali ambazo umeziacha? . Kimsingi hayo ni maswali ya msingi ambayo unatakiwa kujihoji kwa sababu wengi huwa hatujiandai kimaisha kwa ajili ya vitu hivyo.
Wengi huwa tunaishi maisha ya sasa pekee na kusahau kuwa kuna maisha mengine baada ya hayo tunayoishi sasa.
Ikiwa tunataka kuishi maisha ya furaha yasiyokuwa na majuto, pia yenye kutufanya tuone thamani yetu katika dunia hii, tunapaswa kujiandaa kuanzia sasa ili tuje kuishi maisha yenye furaha hapo baadae tukizeea au wakati mwingine kuziacha familia zetu ziishi maisha mazuri pale ambapo sisi tunakuwa hatupo.
Na ili jambo hilo liweze kukamilika tunakiwa kuwekeza vipato vyetu kwa ajili ya uzee wetu na ulinzi wa familia zetu ili familia zetu sizije kuishi maisha magumu hapo baadae.
Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.
0747030303
.png)
0 Comments