BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jinsi ya kuondokana na tatizo la "Over Thinking"

 


Over Thinking  ni ile hali ya mtu kuwa kwenye hali isiyokuwa ya kawaida ambapo mtu huyo anakuwa hajui afanye nini ili aondokane na jambo hilo. 

Au kwa maneno mengine tunaweza kusema Overthiking ni ile ya kuwa na mawazo mengi kichwani na unakuwa huelewi namna unavyoweza kuondokana na mawazo hayo. 

Zipo sababu mbalimbali ambazo hupelekea mtu kuwa katika hali hii ya Over Thinking.  Zipo sababu za kimazingira ambazo zinaweza kukupelea mtu kuwa katika hali hii, sababu hizi huenda ikawa zimetokana na jinsi ambavyo unahusiana na jamii yako.

Kwa mfano labda umegombana na boss wako kazini, au umegombana na mke au mume wako, au yule uliye naye kwenye mahusiano kimapenzi, au wakati mwingine huenda ukawa haupo kwenye mahusiano mazuri na watu wako wa karibu kama vile wazazi, walezi au hata watoto watoto sasa kutoelewa huko kunakufanya mtu uwe kwenye tatizo hili la " over thiking".

Pia huenda tatizo hili likasababishwa na kutokuwa na fedha kwa ajili ya kukidhi hitaji fulani kama vile ada ya wanao, kutokana na tatizo vile unavyowaza jambo hilo ya namna utakavokabiliana nalo ndivyo linakupelekea wewe kuwa katika tatizo hilo la over thinking. 

Au wakati mwingine huenda ukapatwa na tatizo hilo la over thinking kwa sababu mambo yako fulani fulani yanashindwa kwenda sawa, au yanenda tofauti na matalajio yako. Kwa mfano labda ulipanga ndani ya miezi sita uwe umeanza ujenzi, miezi sita imepita na hakuna ulichokamilisha hapo ni lazima utapatwa na tatizo hilo.

Au labda ulikuwa unatalajia kupata mtoto na kwa bahati mbaya mimba imeharibika, moja kwa moja changamoto hiyo itakupeleka kwenye tatizo la Over thiking.

Hizo ni baadhi ya sababu na mifano ambayo hupelekea watu wakapatwa na tatizo hili la over thiking. Wapo baadhi ya watu huchukua maamuzi magumu kila wapatwapo na tatizo hilo.

Wapo baadhi huamua kuwa walevi wa kupindukia huku wakiamini ndiyo njia pekee itakayowasaidia wao kuweza kutoka kwenye tatizo hilo. Wapo wengine huamua kuwa ni watumiaji wa madawa ya kelevya huku nao wakimini kufanya hivyo ni kuondokana na tatizo hilo.

Wapo tena baadhi yao huamua kujiua kwa kujinyonga hiyo yote ni kwa sababu wameshindwa kutafuta suluhu la kuondokana na tatizo hilo la over thinking. 

Wapo wengine pia huchukua maamuzi ya kuwaua wengine ambao waliwasababishia wao wawe katika tatizo hilo. Kwenye kundi hili tumeshuhudia watu walipo kwenye mahusiano ya kimapenzi ndiyo ambao huathiriwa zaidi na athari hii zaidi ya kufanya mauaji.

Kiukweli  zipo athari  nyingi sana katika tatizo hili la Overthing ila hizo nilizozieleza hapo juu ni baadhi tu, sasa ikiwa ukiwa unaathiriwa na tatizo hili unatakiwa kufanya yafuatayo;

Mosi; Kubali kwamba una tatizo hili la over thiking, ni muhimu sana kukubali kwamba una tatizo hilo, kwa sababu unapokubali kwamba upo kwenye tatizo kutasaidia kujua namna ya kutoa kwenye tatizo hilo.

Pili; tafuta njia ya kuondokana na tatizo hilo, kwa mfano kama tatizo lako limesababishwa na ugomvi wako na mke au mume wako basi unapaswa kutafuta suluhu ya namna gani nyie wawili mnapaswa kuelewana. 

Unapopata changamoto inayokupelekea ove thinking kama hiyo ya kugombana na mwenza wako usinywe pombe, Kunywa pombe siyo suluhu, ni suluhu ya muda mfupi ila pombe ikiisha tatizo utalikuta lipo vile vile linakungoja. 

Unachotakiwa kufanya nikutafuta majibu sahihi ya namna ya kuondokana na tatizo hilo.

Tatu; Usiishi kale yako bali ishi leo. Wengi wanasumbuliwa na tatizo hili kwa sababu wameamua kuishi ya kale. Yaani unakuta mtu kitu ambacho kilitokea kipindi cha nyuma ndicho kinachomtesa zaidi ambacho ndicho kilichompelekea kuwa kwenye tatizo hilo.

Sasa naomba usiwe mmoja wapo kwani kufanya hivyo ni kuendelea kuishi kwenye over thinking kwa muda mrefu ambapo kuendelea kufanya hivyo athari zake ni kubwa zaidi, ila unachotakuwa kufanya ni kujifunza kuishi leo.

Yale yote yaliyopita yasiishi ndani yako kwani mara nyingi ndiyo yanayokunyima amani ya moyo, ishi leo itayokufanya utabasamu na kuondokana na tatizo la over thinking. Jifunze kutoka kwa wahenga waliosema yaliyopita si ndwele, ugange yajayo.

Nne; Tumia njia hii kupumua hii ni ya kisakolojia zaidi. Mbinu inakutaka kila wakati ukiwa katika hali hii ya over thinking pasi uvute hewa mara tatu ndani, na upumue mara tatu tena nje. Fanya mara kadhaa kila unapopatwa na hali hiyo ya Over thinking. 

Huenda kwako ikaonekana kama ni mchezo wa kipuuzi ila ndiyo tiba yenyewe ambayo imekaa kisaikolojia zaidi, njia hiyo imewasaidia wengi nikiwemo na mimi mwenyewe. Itumie ikusaidie.

Kwa nukta hiyo sina la ziada nikutakie siku njema na utekelezaji mwema na Mungu akubariki sana.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya. 
0747 030303

Post a Comment

0 Comments