Ulimwengu wa sasa umesongwa na tatizo la watu wengi kutokuwa na furaha. Zipo sababu mbalimbali ambazo zimepelekea kwa kiwango kikubwa kuwapo kwa tatizo hilo.
Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na uwepo wa hali ngumu ya maisha, kuishi tofouti na matarajio yetu, kufeli kwenye mambo ambayo tuliyategemea, uchumi kuyumba, mifarakano baina ya wanajamii na watu wetu wa karibu wanaotuzunguka na sababau nyinginezo ambazo huiba furaha zetu.
Pamoja na uwepo wa tatizo la kutowepo wa furaha katika maisha yetu, zipo athari ambazo hutokana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kupungua kwa ufanisi wa utendaji wetu wa kazi mbalimbali, kuishi maisha mafupi, wakati mwingine huleta madhara ambayo hutupelekea kupata magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo tatizo la afya ya akili na magonjwa mengineyo.
Pamoja na ukubwa wa tatizo hilo la watu wengi kuwa na tatizo hilo la kutokuwa na furaha, kumekuwa na uhaba pia wa watu kutokujua namna sahihi ya kuondokana na tatizo hilo, lakini makala haya yatakusaidia ili uweze kuondokana na tatizo hilo kama ifuatavyo;
1. Yakubali maisha yako unayoyaishi kwa sasa.
Wapo baadhi ya watu wamekosa furaha maishani kwa sababu kuna wakati walikuwa wanaishi maisha ya hali fulani ila kwa sasa maisha wanayoyapitia ni tofauti na hapo awali. Kitendo hiki kimewapelekea watu hao kukosa furaha kabisa katika maisha yao.
Sasa ikiwa na wewe ni miongoni mwa watu hao ipo haja kubwa ya kuyakubali maisha ambayo unayoishi, huku ukiendeleza harakati zako za upanambaji ambazo zitakufanya uwe na furaha.
Yawezekana pia, ulifeli katika jambo fulani ambapo kufeli huko kumekusababisha wewe kutokuwa na furaha, basi nawe ipo haja ya kukubali kwamba ni kweli ufeli na kufeli kupo tu, hivyo unatakiwa kuendelea kupambana ili kufeli huko kusijirudie tena.
2. Fanya kitu kitakachowasaidia wengine.
Wakati mwingine unapopitia hali ya kutokuwa na furaha basi jifunze kufanya kitu ambacho moyo wako unapenda kukifanya ambacho kitawasaidia wengine pia.
Watu wenye uhitaji na kitu fulani ni wengi sana, hivyo kama kitu hicho kipo ndani ya uwezo wako we kifanye ili kiwasaidie wengine pia. Kwa mfano wapo baadhi ya watu ukiwauliza wao furaha yao hutokana na nini? Wengi hujibu furaha yao hutokana na vile wanavyowasaidia watu wengine.
Kwa mfano hata mimi mara nyingi furaha yangu kubwa kutokana na vile yale ninayoandika yanavyowasaidia wengine, nikipata mrejesho namna maandikio yangu yanavyowabiriki wengine, ndivyo ambavyo furaha yangu huwa ni kubwa zaidi.
Wasaidie wengine lile lililo ndani ya uwezo wako hili litakusadia nawe ili furaha zaidi katika maisha yako.
3. Jifunze kusamehe.
Ili uwe na furaha katika maisha yako unatakiwa kujifunza kusamehe. Kusamehe kupo kwa aina mbili, mosi kujisamehe wewe mwenyewe katika makosa ambayo uliwahi kuyatenda, pili kuwaseheme wengine ambao waliwahi kukukosea.
Unapowasehe wengine ambao waliwahi kukukosea ni tiba ya moyo, kwa sababu unapowaseheme wengine unakuwa unatua mzigo ambao upo ndani ya moyo wako, hivyo unaufanya moyo wako kuwa na amani pia. Unapokuwa na amani ndani ya moyo wako ndivyo furaha yako inavyojitengeneza yenyewe pia.
Unapaswa kujisamehe wewe mwenyewe kisha kuwaseheme watu wengine ili uweze kuwa na furaha na amani ndani ya moyo wako. Msamaha ni tiba ya kukuletea furaha maishani.
Mwisho niweke nukta kaa kusema ya kuwa, kwenye maisha haya ya kila siku ambayo tunayaishi mimi na wewe furaha ni kitu muhimu sana ambacho hatupaswi kukikosa kwani kina mchango mkubwa sana wa maendeleo yetu binafsi na maendeleo ya taifa leo kiujumla.
Furaha ni kila kitu maishani.
Na Afisa mipango Benson Chonya.
.png)
0 Comments