BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Sababu za watu kuwa na madeni.

 


Maana halisi ya Deni ni mkopo uliopitiliza. Ukiona umekopa mahali na mkopo huo ukashindwa kurejesha ndani ya wakati mliokubalina ni hilo ndiyo deni.

Idadi kubwa ya watu wanasongawa na madeni katika maisha yao. Wapo wanadaiwa na watu binafsi kama vile ndugu, jamaa na marafiki, wapo wanaodaiwa na ofisi zao, wapo wanaodaiwa na serikali, wapo wanaidawa na taasisi za kifedha, wapo wanaidaiwa na vikundi.

Zipo aina mbili za madeni ambayo ni  madeni mazuri na madeni mabaya.

Madeni mazuri ni yale madeni ambayo mtu ukikopa unalipa kwa wakati pia unafanyia mkopo huo vitu vya maana, yaani hapa mkopaji anakuwa hajutii kukopa kwake.

Madeni mabaya ni mkopo ambao unakuwa umepiliza muda wa kulipwa, Pamoja na uwepo wa madeni hayo, wengi wanavyokopa hawakujua kama litakuja kuwa ni deni ambalo litakuwa linamsumbua kwenye ulipaji, hadi kufikia hatua  kuwakimbia wadeni wao. 

Wengi walidhani pindi watakavyokopa huenda wakalipa mapema zaidi lakini mambo huenda kuwa ni kinyume chake. Pia aina hii ya madeni huwafanya watu kuwa wanyonge kwani mkopo huo hutumia vibaya hata ulipwaji wake huwa ni changamoto.

Tuangalie sasa sababu za madeni;

Kutumia hela ambayo haupo nayo mkononi.

Watu wengi hujikuta wamedondokea kwenye madeni kwa sababu tu ya kufanya matumizi ya pesa ambayo hawapo nayo mkononi.

Kwa mfano, mtu anakuwa ana matumaini ya kupata hela sehemu fulani, hivyo anamua kukopa kitu fulani huku akiamini kuwa ile hela ikija atalipa, hivyo hela hiyo isipokuja kama mtu huyo alivyotaraji anajikuta ameingia kwenye mkopo usiyotarajiwa.

Kutumia zaidi ya kipato chako.

Hii ni sababu nyingine ambayo huwapelekea watu wawe kwenye madeni. Mtu ana kipato kidogo ila anafanya matumizi zaidi ya hicho kipato chake, mwishowe anadondokea kwenye madeni.

Kwa mfano, unaweza kukuta mtu kipato chake ni shilingi mia tano, ila anatumia shilingi mia saba, hilo ongezeko la shilingi mia mbili na hela ambayo siyo yake. Hivyo mtu huyo anajikuta kila siku anakopa ili kuweza kukidhi hitaji fulani.

Maisha hayo yapo sana kwa watu wengi. Wengi tunapenda maisha ya juu au wakati mwingine kuonyesha ufahari wetu kwa watu wengine, ili kufaanya hivyo tujaikuta tunakopa pasipo kuwa na sababu hivyo kutupelekea sisi kuishi zaidi ya kipato chetu ambacho hututengezea madeni.

Kutokuwa na utaratibu wa kutenga fedha ya dharula.

Hii nayo ni sababu nyingine, wengi tunapopatwa na majanga ambayo hatukuyategemea hujikuta tunakimbilia kukopa, kukopa huko hutufanya tuingie kwenye madeni hiyo yote kwa sababu hatukuwa na utaribu wa kuweka akiba kwa ajili ya dharula.

Kwa mfano, umeugua ghafla na hauna hela ambayo huwa unaiweka kwa ajili ya dharula, unadhani ni kitu gani kitatokea, moja kwa moja utaenda kukopa.

Mambo ya ghafla hutuingiza kwenye madeni kila siku.

Hivyo ili usiwe na madeni unatikiwa kufanya yafuatayo; kutenga fedha kwa ajili ya dharula kwa  njia ya kuweka akiba, kila wakati epuka kutumia zaidi ya kipato chako, jifunze kuishi chini ya kipato chako na usipende kufanya matumizi kwenye hela ambayo haupo nayo mkononi.

Na afisa mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments