BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Njia zitakazokusaidia kuondokana na umaskini.

 


Umaskini wa kipato ni umaskini ambao unayatafuna maisha ya wengi wetu, wengi tumejikuta tukisema kuwa kila kukicha ni afadhari ya jana, hii ni kwa sababu tumekuwa hatukioni kivuli cha kuyapoza maumivu tunayoyapitia.

Pamaja na uwepo wa hali hiyo ya umaskini, tumeingia kwenye imani za kuamini huenda wale wenye mafanikio ndiyo wameumbiwa kuwa hivyo, au wakati mwingine tunazidi kuamini kuwa wale waliofanikiwa mara nyingi wamekuwa hawatumii njia za halali kuyapata mafanikio hayo.

Na ukweli ambao upo wazi ni kwamba mafanikio hayo yamezidi kutupita kwenye vichwa vyetu kwa sababu ya imani tulizojiwekea. Ila ukweli ni kwamba hakuna mafanikio ya watu wachache, bali mafanikio ni ya watu wote.

Hivyo ili kuondokana na hali ya umaskini tuliyonayo tunakiwa kufanya mambo yafuatayo;

1. Wekeze muda mwingi kwenye kusoma vitu vitakavyotujenga.

Mafanikio yamefichwa katika maandishi, kile ambacho kinakusumbua kichwa chako kipo kwenye maandishi ni suala la kutafuta maandishi hayo ili yaweze kukusaidia. 

Kama unataka kuwa kinara wa jambo fulani tafuta kitabu kinachokusiana na jambo hilo kisha kisome kitabu hicho ili kikusaidie kukupa majibu ya maswali yako unayoyatafuta.

Kama umekuwa na changamoto ya malezi, tafuta vitabu vya malezi vikusadie, kama una changamoto ya kuweka akiba tafuta vitabu vinavyofundisha namna kuuanza kuweka akiba, kama una changamoto ya madeni maishani mwako basi tafuta vitabu vitakavyokusaidia kukutoa katika madeni hayo.

Si vitabu tu, bali tafuta video ambazo pia zimeelezea majibu ya changamoto unazozipitia ili viweze kukusaidia.

2. Anza kuamini wewe mwenyewe kwanza.

Mara nyingi watu wengi tumekuwa hatuna imani chanya juu ya mambo fulani, wengi tuna imani nusunusu, wengi imani zetu ni hasi na ndizo zinazotuchelewesha zaidi.

Hatuamini kama mambo yanawezekana, hatuamini katika kufanikiwa kwa njia halali, wengi tunaamini katika imani za kishikirikana, wengi hatuamini katika upambanaji ulio halali wa kiutafautiji, imani hizi ndizo zinazotuchelesha zaidi.

Ila ukweli ambao upo wazi  lazima tupeane ni kwamba kila kitu kinawezekana endapo tutaweka mitazamo yetu katika kuanza kuamini sisi wenyewe kwamba kila kitu kinawezekana. Pia tunaanze kuamini kuwa mafanikio ni haki ya kila mmoja wetu.

3. Usiwe na visingizio.

Uwepo wa visingizio maishani unatufanya maisha yetu yaendelee kuwa yale yale kila uchwao. Hii ni kwa sababu mtu wenye visingizio vingi maishani si mtu wa utekelezaji isipokuwa ni mtu mzuri wa kugharisha kufanya vitu vya msingi.

Wenye visingizio huwa hawakosi sababu, utawasikia mara oooh mimi sina hela, mala mimi yatima, mara mimi sijasoma hivyo nashindwa kufanya jambo fulani.

Huku wemesau kuendelea kuvishikilia visingizo hivyo maishani mwao ni kuendelea kujichelewesha wao wenyewe. 

Ila ukweli kitu pekee kinachotakiwa kufanya ili kuepuka na visingizo hivyo ni kuachana na sababu zisizokuwa za msingi na kuanza mara moja kutafuta njia za kutekeleza jambo hilo.

4. Jitoe muhanga.

Kila wakati kama umechoshwa na hali ya umaskini unayoipitia jifunze kujitoa muhanga. Jitoe muhanga katika kufikiri kwako. 

Jitoe muhanga katika kujifunza vitu vipya, Anza kuamini katika mawazo chanya pia, badili tabia mbaya kwenda kuwa tabia nzuri zitakazokusaidia kupata matokeo unayoyataraji.

Jitoe muhanga kutoka kwenye maeneo uliyozoea ambayo yanakufanya uzidi kuchelewa na uende kwenye maeneo yatakayokujenga zaidi.

Jitoe muhanga katika kupambania ndoto na malengo yako uliyojipangia ili uweze kufanikiwa zaidi.

Ukiyazingatia mambo hayo manne ni ukweli ulio wazi kwamba maisha yako yatakwenda kubadilika sana na utaondokana na hali ya maskini uliyonayo.

Ndimi afisa Mipango Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments