Idadi kubwa ya watu imetawaliwa na hofu ya kutokujiamini. Wengi wamejawa na wasiwasi mioyoni mwao na hiyo yote ni kwa sababu ya kutokujiamini.
Wengi hawajiamini kwenye mawazo hata matendo yao. Watu hao pia wamekosa uwezo wa kuonyesha yale mambo makubwa waliyonayo hii yote ni kwasababu wamekosa kujiamini.
Wengi wao wanawaza namna watu wengine watakavyowachukulia, wengine pia wamekosa hamasa ya kuanzisha jambo fulani, wapo wale waliokosa ule uwezo wa kuzungumza mbele ya watu wengine pia.
Ikiwa hata wewe unayesoma maandishi haya una tatizo hilo la kutojiamini basi unatakiwa kufanya mambo haya yafuatayo;
Anza kufanya kile kinachosababisha usijiamini.
Kama kuna jambo ambalo limekuwa linakufanya ukose kujiamini basi unatakuwa uanze kufanya jambo hilo mara moja sasa hivi.
Kama ulikuwa huwezi kuongea mbele za watu anza sasa hivi kuzungumza. Kama kuna biashara ulikuwa unatamani kuifanya ila ukawa unakosa ile hali ya kujiamini unachotakuwa kufanya ni kuanza mara moja kuifanya biashara hiyo.
Kwenye kila eneo ambalo lilikuwa linakufanya ushindwe kujiamini, basi unachotakiwa kufanya kuanza mara moja kufanya kile ambacho kilikuwa kinakufanya ukose kujiamini kwako.
Fanya vitu mara kwa mara.
Ili uweze kujiamini zaidi kitu kingine unachotakiwa kuanza kukifanya ni kufanya vitu mara kwa mara. Unapofanya vitu mara kwa mara ubongo wako, utakufanya utoke kwenye lile shimo la kutokujiamini na sasa utaanza kujiamini.
Unapofanya vitu mara kwa mara akili hugeuza yale uliyokuwa haujiamini nayo kuwa sehemu ya tabia yako. Kwa mfano kama una tatizo la kutoa maoni yako mbele ya watu wengine, unapokaa na watu hao na ukaanza kuongea mara kwa mara ni kwamba utaanza kuijenga hali mpya ya kujiamini ambayo mwanzo ulikuwa haupo nayo.
Nakumbuka hata mimi wakati naanza uandishi nilikuwa sijiamini kabisa ila kadri siku zinavyozidi kwenda nikawa naandika mara kwa mara mwishowe nikajikuta ubongo wangu umeanza kujenga hali ya kujiamini na hali hiyo nipo nayo mpaka kesho kutwa.
Hivyo hata wewe nahusihi sana kama una tatizo la kutokujiamini ni heri utumie njia hizi zitakazokusaidia kujenga hali ya kujiamini. Kwani endapo utaanza kujiamini utafanya mambo makubwa ambayo mwanzo ulikuwa unayaogopa.
Ndimi afisa mipango Benson Chonya.
0747030303
.png)
0 Comments