BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kumbuka jambo hili kwenye biashara.

 


Wafanyabiashara wengi  wanapenda kuwajiri watu ili watu hao waweze kuwasaidia katika majukumu mbalimbali ya utendaji wa kazi.

Kumuajiri mtu akusaidie kazi mbalimbali hilo siyo tatizo ila tatizo linakuja  kwenye utendaji wa kazi hiyo. Usimuajiri mtu kisha kumuacha mtu huyo aendelee na kazi pia kufundisha vitu muhimu kuhusu biashara yako.

Mmiliki wa biashara yeyote ile kumbuka  unapomuajiri mtu unatakiwa umfundishe huyo mfanyakazi wako kuhusu biashara hiyo, yaani hakikisha muuzaji/mfanyakazi wako anakijua kile unachokijua kuhusu bidhaa au huduma yako.

Nasema hivyo kwa sababu mara nyingi, wafanyakazi wengi wanashindwa kuuza kwa sababu kile wanachokiuza hawakijui vyema, na tatizo hilo linaanzia kwako ambaye hujataka kumfundisha mfanyakazi wako kuhusu biashara hiyo.

Kila wakati weka muda mwingi kumfundisha kuhusu kile unachokijua kuhusu biashara hiyo, eleza kwa kina kuhusu namna bidhaa hiyo inavyofanya kazi, eleza uzuri wa kitu hicho pia mueleze mfanyakazi faida atakazopata mteja mara baada ya kununua bidhaa fulani na jambo hili ni muhimu.

Ni muhimu sana jambo hilo, kwa sababu wateja tunanunua faida za kitu fulani, yaani kwenye kila kitu tunachonunua tunategemea kupata faida fulani kutoka kwenye kitu hicho. Hivyo unapomuajiri mtu mfundishe jambo hilo.

Ukifanya  jambo hilo la kumfundisha mfanyakazi wako kile unachokijua ni lazima utapata matokeo makubwa kwenye biashara kwa sababu hata usipekuwepo biashara itafanyika vizuri kwa sababu mfanyakazi wako atakuwa anaweza kuelezea vizuri kile unachokijua kwa wateja.

Na; Benson chonya.

Post a Comment

0 Comments