BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hivi ndivyo unavyoweza kuondokana tabia ya uvivu.

 



Uvivu ni sababu nyingine ambayo inatukwamisha wengi wetu kupata matokeo sahihi kwenye yale mambo yetu ya msingi tuyafanyayo. Zipo sababu mbalimbali ambazo hutupekelewa watu wengi kuwa ni watu wavivu, miongoni mwa  sababu hizo ni pamoja na kufanya vitu tusivyopenda na sababu nyinginezo.

Sasa ikiwa wewe ni mtu ambaye ni mvivu  basi unatakiwa kufanya mambo haya yafuatayo ili uweze kuondokana na uvivu huo;

1. Kuwa na shauku ya kufanya kitu unachokipenda.

Mara nyingi uvivu wa mtu hutokana na kufanya kazi kwa kutoipenda kazi hiyo. Mtu anapoifanya kazi asiyoipenda huwa shauku yake ya kutendaji wake ya kufanya kazi hiyo huwa ipo chini sana, kila akitaka kuifanya kazi hiyo anaingiwa na uvivu.

Hivyo ili usiwe mtu mvivu wa kufanya kazi fulani, basi kila wakati unatakiwa kuwa  na shauku ya kufanya kitu unachokipenda. Ukifanya kitu unachokipenda hata uwe mvivu kiasi gani uvivu huo huo unapotea mwenyewe.

2. Wekaza jitihada katika kazi yako.

Ili usiwe mtu mvivu katika jambo lolote lile utakiwa kuweka jitihada za utendaji wako wa kazi. Jitihada hizo zinaweza kuwa jitihada za akili, jitihada za nguvu, jitihada za muda na jihitahada zako za kipesa.

Ukiwekeza jitihada za vitu hivyo ni lazima utakuwa ni mtu ambaye unafanya kazi kwa juhudi zako kwa sababu asilimia kubwa ya vitu ambavyo huleta matokeo fulani umewekeza vyote kwenye jambo husika. Hiyo uwekezaji wa mambo hayo yatakufanya usiwe mvivu kwenye kazi zako.

3. Usifanye kazi muda wote, jipe muda wa kumpumzika pia.

Inapotokea ukaona akili yako imechoka hasa pale unapofanya kazi zako wala usione aibu kuipa akili yako na mwili wako muda wa kufanya mapumziko.

Unapopumzika unakusanya nguvu za kiutendaji wa kazi fulani, hivyo inapotoea unaonea umechoka kufanya jambo fulani wala usione tabu, wewe pumzika. Unapopumzika  kisha kurudi tena kwenye kufanya kazi ni lazima tu kama ulikuwa na tabia ya kivivu tabia hiyo itaisha yenyewe.

4. Usiwe na mlundikano wa kazi kwa wakati mmoja.

Wakati mwingine ili usiwe mvivu unatakiwa usiwe mtu ambaye unalimbikiza kazi. Akili ya mwanadamu huingiwa uvivu wa kiutendeaji ikiwa mtu huyo akiwa na tabia ya kulimbiza kazi kwa wakati mmoja.

Hivyo ili uondokane na uvivu, weka ratiba yako vizuri ya kufanya kazi, kila kazi iwe katika mpangilio, usianze kufanya kila kazi ambayo haikuwa kwenye ratiba yako kwa sababu ukiwa mtu wa namna hiyo utakuwa unalimbikiza kazi nyingi ambazo zitakuwa zinakukabali mbele yako.

Ukiyazingatia hayo ni lazima utakuwa ni mtu wa kufanya kazi kila wakati bila kuwepo sababu mbalimbali zinazokuzuia kufanya kazi ikiwepo na sababu ya uvivu.

Ndimi afisa Mipango Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments