BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Biashara ni nini?

 


Siku ya leo naomba nikupe maana tofauti kabisa na ile ambayo wewe umeizoea kuhusu maana halisi ya biashara. Wengi tunafahamu kwamba biashara ni mabadilishano ya bidhaa kwa bidhaa au mabadilishano ya bidhaa kwa fedha.

Ila leo nakuongezea maana nyingine ya neno biashara kwamba, Biashara ni vita ya mtazamo. Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara yoyote ile ni lazima uweze kushinda kwenye mitazamo ya watu kuhusu kile wanachokijua kuhusu wewe.

Kwa mfano, leo hii kuna baadhi ya makampuni yanayouza simu ambazo ni nzuri sana, ambazo ni imara, haziharibiki mapema, kila mmoja anatamani kuwa nazo simu hizo na simu hizo hata zipande bei vipi, ila watu huwa wananunua tu.

Lakini zipo pia baadhi ya makampuni ya simu, hata watengeneze simu nzuri kiasi gani watu huwa hawanunui kwa wingi kwa sababu wao wanaamini kuwa simu hizo huwa ni feki, pia huwa zinaharibika mapema.

Hiyo ndiyo maana halisi ya vita ya mtazamo wa wateja katika biashara yako. Kila wakati uza vitu ambavyo watu watakuwa na mtazamo chanya juu kile unachokiuza.

Haijalishi unafanya biashara gani, bali kwenye kila eneo  la biashara yako waza namna watu watakavyowaza chanya kuhusu biashara yako.

Watu wakiwaza vibaya kuhusu kile unachokifanya ni lazima watu hao watapotea tu. Watu wakiwa na mitazamo kwamba biashara yako ni mbaya ni lazima itakuwa mbaya kila siku. Ila watu wakiwa na mitazamo kwamba biashara yako ni nzuri ni kweli biashara hiyo itakuwa nzuri tu.

Pia watu wakiwa na mitizamo chanya kuhusu biashara unayoifanya, ni lazima watu hao watakuja tu kwako kama wateja. 

Pia wateja huwa wana tabia ya kusambazina uzuri kuhusu wa kitu fulani. Hivyo ukiuza kitu kizuri ni lazima watu watasambaziana uzuri wa  kitu hicho, hivyo mwishowe utajikuta biashara yako inafanya vizuri zaidi.

Lakini pia ukiuza kitu kibaya, ni ukweli kwamba kitu hicho pia hakitafanya vizuri kwa sababu watu watasambazina pia kuhusu ubaya wa kitu hicho.

Unakumbuka ule usemi usemi" kizuri chajitangaza"  kama unakumbuka basi kila wakati waza utavyoweza kukaa kwenye vichwa vya wateja kuhusu uzuri wa kile ukifanyacho, ukifanikiwe kwenye hili kila kitu kitakwenda salama kabisa kwa sababu utashinda kwenye vita ya mtazamo.

imeandikwa na Benson Chonya.

Post a Comment

0 Comments