BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Ijue nguvu ya ukimya kwenye maisha.

 


Kwenye maisha unapaswa kutambua nguvu iliyopo kwenye ukimya, mwingine anaweza kuuliza ukimya maana yake ni nini, je ni kutokuongea? Hapana hiyo siyo tafsiri sahihi ila ukimya ni siyo kila sehemu unapaswa kuongea, isipokuwa ukimya ni ile hali yakuchagua uongee nini, uongee wapi na kwa wakati gani.

Ukiwa muongeaji sana watu watashindwa kukupa muda wao kukusikiliza, kwa sababu wengine huwa hatupendi mtu muongeaji sana. Hivi hujawahi sikia watu wakisema aaah tatizo jamaa ni myongeaji sana.

Je unadhani sentesi hiyo ni sifa nzuri? Hapana si sifa nzuri, bali unapaswa kujifunza kuwa unachugua uongee  nini na kwa wakati gani, ukijifanya muongeaji wa kila kitu watu watakuweka lile kundi la mtu mjuaji kwa kingereza huitwa ( much know). Much know ni aina ya watu ambao hujifanya wao kila kitu wanakijua. 

Tafadhari sana kuitwa mjuaji  (much know ) si sifa nzuri kwa sabau wapo baadhi ya watu watakuwa hawakuamini kwa ile hali uliyonayo wengi watajua wewe ni muongo muongo.

Unachotakiwa kufanya ni kuwa mkimya kwa sababu ukiwa mkimya kuna faida hizi;

1. Watu watakuamini sana.

Ukiwa si mtu wa kuzungumza sana watu watakuwa wanakuamini sana kwa sababu mtu ambaye anachagua ni wapi aongee na aongee nini, mtu huyo ana nafasi kubwa ya kuaminika katika jamii kuliko wale watu ambao wanaongea sana.

Hivyo ili jamii yako iweze kukuamini basi unatakiwa uchague kuwa mkimya kwa sababu jamii huamini watu ambao ni wakimya.

2. Utakuwa ni mtu mwenye mawazo mazuri.

Ukiwa mkimya tafsiri yake ni kwamba wewe utakuwa ni mtu mzuri ambaye unasikiliza pia. Kwa nukta hiyo ni ukweli ulio wazi muda mwingi kabla ya kuongea utakuwa ulipata wakati mzuri wa kusikiliza kwanza.

Hivyo unatakuwa na mawazo mazuri ambayo utakuwa umeyapata kutoka kwa watu wengine walivyokuwa wanaongea, hivyo utajua ni kitu gani unachotakiwa kuzungumza na kwa wakati gani, na pia ni kitu gani ambacho hutakiwi kuzungumza.

Kila wakati jifunze kuwa mkimya kwa sababu ukimya ni chumba kizuri cha kukupa mawazo mazuri sana, kwa sababu muda mwingi utakuwa na wakati mzuri wa kutafakari juu ya nini kinachotakiwa kusemwa na kufanyika pia.

3. Ukimya huongeza umakini kwenye jambo (focus).

Unapokuwa mkimya basi huongeza umakini kwenye mambo yako. Ukiwa mkimya utakuwa huyumbishwi na mambo yanayoendelea katika ulimwengu huu.

Bali wewe utakuwa ni mtu ambaye unasimia kwenye kutimiza maono yako zaidi. Hivyo kila wakati jifunze kuwa mkimya ili uweze kuongeza umakini wako zaidi.

Imeandikwa nami Benson chonya.
0747030303

Post a Comment

0 Comments