BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Siri ya kupata mafanikio ya kudumu.

Uwazi unajenga uaminifu. Kwa kila unachofanya, kuwa na uwazi wa asilimia 100. Usifiche kitu chochote kwenye biashara yako, mweleze mteja ukweli kuhusu kile unachomuuzia yeye.

Kama ikitokea ukimdanganya mteja wako kuna siku atakuja kujua na utaharibu kabisa mahusiano yenu ya kibiashara. Weka uwazi na kuwa mwazi ili ufanikishe mambo mengi sana.

Kuna watu wanakuwa sio wawazi, na matokeo yake, wanakuwa wanafanya biashara ya mara moja, na hawawezi tena kuwapata wateja hao kwa sababu hawakuwa wawazi.

Siri ya kupata mafanikio ya kudumu kwenye maisha na biashara ni kuamua kuwa mwazi. Ukiweka uwazi, kila kitu kitaenda sawa. Moja ya msingi mkubwa wa mafanikio, ni uwazi.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments