Kila wakati ni muhimu kuelewa kwamba maisha ni magumu sana hivyo ili kuweza kuondokana na ugumu huo basi tunatakiwa kuwa ni watu ambao pamoja na ugumu huo tuwe ni watu wa kutafuta suluhisho kwenye yale yanayototokea.
Changamoto ni nyingi sana katika jamii yetu hivyo wajibu wetu ni mmoja tu kwenye kila changamoto ambayo tunakumbana nayo ni muhimu sana kuweza kutafuta majibu na namna ya kuondokana na changamoto hizo.
Mtalaam mmoja aliwahi kusema kama itatokea umelala na njaa hautakiwi kulalamika juu ya kulala na njaa bali unatakiwa kutafuta sababu ya kulala na njaa. Kama ilivyo katika mfano huo wa njaa basi hata wewe kwenye kila changamoto inayojitokeza mbele yako hautakiwi kulalamika bali unatakiwa kutafuta suluhisho la kutatua changamoto husika.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.

0 Comments