BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Jinsi ya kuwa makini na matumizi yako ya fedha.


Unapokuwa na vitu au pesa acha kuchukulia rahisi, au poa kwamba kila mtu ana uwezo wa kuwa nazo na unatumia na kila mtu. Unapokuwa na pesa jenga kichwani mwako falsafa ya ugumu, falsafa ya kutokuruhusu pesa zako zitumike hovyo.

Hapa sasa, ndio utatakiwa kuwa makini na watu wote wanaokuzunguka, wale watu ambao wanaona pesa zako kama zao na kuzitumia kama wanavyotaka na halafu wewe pia unajiachia. Watu wana mambo wanakupenda unapokuwa nazo.

Hapa sasa, ndio unatakiwa kuwa makini sana na matumizi yako ya pesa ya kila siku na kuyalinda yasiwe ya hovyo kwako na ukajuta. Weka akilini mwako kwamba, ukipoteza pesa zako kirahisi, kuzipata kwake tena, itakuwa ngumu kwako.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments