BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mambo utakayojifunza kutoka kwenye kitabu cha Secret of Ages cha Robert Collier.

 


Masomo tisa utakayojifunza kutoka kwenye kitabu cha Secret of the Ages kilichoandikwa na Robert Collier.

1. Sheria ya uvutano ni kitu halisi.  Sheria hii ya uvutano inasema kuwa kile unachokifikiri ndicho utakachokipata. Hivyo wekaza akili yako kwenye vitu chanya ili uweze kuvivuta vitu hivyo unavyovitaka vije katika maisha yako. Anza mara moja kuamini kwenye mambo yanayowezekana ili mambo hayo yaweze kuwa kitu ukitakacho.

2. Akili yako ina uwezo wa kufanya mkubwa sana. Mwandishi anasema akili yako ikitulia katika kufanya kazi zake vizuri ina uwezo mkubwa wa kubadili mawazo yako kuwa kwenye kitu halisi. Hivyo unapaswa kuiruhusu akili yako iwaze mambo chanya yatakayokupa mafanikio uyatakayo.

3. Hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako. Kwa kuwa wewe ndiye mmiliki wa maisha yako basi ni lazima utambue nguvu ya kuchagua mawazo yako, kwa kuangalia ni mawazo yapi yanafaa na mawazo yapi hayakufai. Unapochagua mawazo yako hakikisha unayaweka mawazo hayo kwenye matendo, kwani kuwaza bila kuweka yale unayoyawaza kwenye matendo ni kazi bure.

 4. Wasaidie wengine na itakusaidia kujisaidia wewe mwenyewe. Kanuni ya mafanikio inasema kuwa unapowasaidia wengine unajisaidia wewe pia, hii kwa sababu Mungu huwabariki sana wale ambao huwasaidia wengine pia hivyo kupitia kuwasaidia wengine unakuwa umejisaidia pia, unapowasaidia wengine unajizolea baraka nyingi kutokana msaada huo unaoutoa.

5. Ishi wakati uliopo. Wakati uliopita umepita na wakati ujao bado haupo mikononi mwako, kwa hiyo hakikisha unaishi wakati uliopo na ufurahie wakati huo. Wapo baadhi ya watu wanashindwa kufanya makubwa kwa sababu ya kuendelea kuishi nyakati ngumu zilizopita ambazo hazina maana yeyote ile maishani mwao. Narudia tena jifunze kuishi wakati uliopo.

6. Shukuru kwa kile ulichonacho. Baraka za mafanikio huenda kwa mtu ambaye hushukuru kwa kile alichonacho, unaposhukuru kwa kile ulichonacho unapata baraka zitakazo kufanya uweze kupata vitu vizuri zaidi kwenye maisha yako. Haupaswi kulalamika kwa hicho ulichinacho maana kitu hicho ni kikubwa sana, maana kuna mtu mwingine hana kabisa kitu hicho.

7. Usigope changamoto. Unapoogopa changamoto utakuwa muoga wa kafanya mambo mengi sana kwa sababu kila kitu unachotaka kufanya utakuwa na uoga wa kufanya kitu hicho. Pia ikumbukwe ili uweze kufanikiwa zaidi na zaidi ondoka mara moja kwenye maeneo uliyoyazoea yanakukwamisha kuweza kufanikiwa.

 8. Jiamini mwenyewe. Kitu muhimu unachopaswa kuwa nacho katika maisha yako ni kujiamini wewe mwenyewe. Kama utajiamini wewe mwenyewe unaweza kufanikiwa kwenye vitu vingi. Anza sasa kuamini kwenye mawazo yako, amini kwenye matendo yako ili uweze kufanikiwa. Ukishindwa kujiamini wewe mwenyewe ni kwamba mambo mengi yanayohusu mafanikio yatakuwa hayapo upande wako.

9. Usikate tamaa kwenye ndoto zako. Haijalishi ni mambo magumu kiasi gani unakutana nayo, kamwe usikate tamaa kwenye ndoto zako bali endelea kupambana kila wakati mpaka pale utakachokitaka kiwe kimekamilika. Tunafahamu vikwazo vipo vingi sana kwenye maisha haya, pamoja na vikwazo hivyo basi endelea kupambania ndoto zako.

Ni matuimini yangu makubwa kuna jambo umejifunza kupitia uchambuzi huo, Asante kwa kusoma na Mungu akubariki sana.

Jumapili ijayo nayo ni siku, tukutane siku hiyo kwenye uchambuzi mwingine.

Ndimi Afisa Mipango Benson Chonya. 

Post a Comment

0 Comments