BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Linda mtaji wako usipotee kwa kufanya haya.

Ili uweze kulinda mtaji wako usipotee, unashauriwa sana kuwekeza kwenye mradi/miradi yenye kuleta faida. Ukifanya hivyo ni lazima fedha zako zitakuwa salama kwa sababu mtaji wako utaongeza  na utaona faida kwenye kile ulichowekeza.

Wakati mwingine swali linaweza kuwa, je nitajuaje kuwa mradi huu utaleta faida? Majibu ya swali hilo ni mepesi kabisa! Kwamba kabla hujaamua kufanya uwekezaji wa pesa zako kwenye jambo ambalo lolote lile, unatakiwa kujiridhisha vya kujosha kuhusu changamoto na fursa ambazo zipo kwenye jambo hilo kabla hujaamua kuwekeza. 

Usiwekeze kwenye jambo lolote lile kutokana na hamasa ambazo unapewa kutoka kwa marafiki zako, ukifanya hivyo huenda ukapoteza bure mtaji wako. Jambo pekee ambalo unapaswa kulifahamu ni kuamua kujifunza kwa kina kwenye kile unachotaka kuwekeza. 

Imeandikwa na afisa mipango Benson Chonya.
0747030303

Post a Comment

0 Comments