Ili mtaji wako uwe salama zaidi kabla hujaamua kufanya uwekezaji wa aina yeyote ile amini ya kuwa kile unachokijua wewe hakitoshi bali unatakiwa kujifunza kwa watu wenye uzoefu na kitu hicho.
Na njia pekee itakayokusaidia kuweza kujifunza kutoka kwa wazoefu hao, ni kuwatafuta wazoefu hao ili waweze kukuelekeza kile ambacho wao wana uzoefu nao.
Kama unataka kupata uzoefu kwenye uwekezaji wa biashara ya mkaa ni lazima umtafute mtu ambaye tayari ana uzoefu au ambaye anafanya biashara hiyo.
Ukiamua kujifunza biashara ya kuuza mkaa kwa muuza nyanya huenda ukapata majibu na hamasa za uongo zaidi kwa sababu mtu huyo hana uzoefu wa kutosha juu ya biashara ya kuuza mkaa.
Hivyo ili uweze kulinda mtaji wako kabla ya kufanya uwekezaji wowote ule uliza kuhusu kile unachotaka kuwekeza kwa mtu sahihi, kwani uwekezaji wowote ule bila taarifa sahihi ni hasara ya kiwango cha lami.
Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya.
.png)
0 Comments