BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kitu hiki ndicho hupoteza fedha za watu wengi.

Miongoni mwa sababu ambazo hupoteza fedha za watu wengi ni pamoja na watu hao kuwa na tamaa ya kuwa na utajiri kwa haraka, kitendo hiki ni kibaya na kimesababisha fedha za watu kupotea bila sababu ya msingi.

Wengi wamekuwa na tamaa za utajiri wa muda mfupi, kwa mfano mtu akishirikishwa kuhusu fursa au biashara fulani kwamba inalipa zaidi mtu huyo pasina kuhoji  faida na changamoto zinazopatikana katika fursa hizo hujikuta aikiingia kichwa kichwa huku akiamini atapata faida.

Kitu ambacho huwa na kinyume chake, sasa ikiwa unataka kulinda fedha zako, acha kuwa na tamaa za utajiri wa haraka, kila kitu unachoshirikishwa kuhusu kitu fulani, kabla hujaamua kufanya uwekezaji wako ni lazima uelewe kitu hicho kwa undani zaidi.

Kwani kama utaamua kufanya uwekezaji wako pasipo kulijua jambo hilo unalotaka kuwekeza basi jiandae kupoteza mtaji wako wote.  Kabla hujafanya uwekezaji wowote ule hakikisha unajua hatari na mapungufu kwenye kile unachotaka kuwekeza.

Imeandikwa na Afisa Mipango Benson Chonya. 

Post a Comment

0 Comments