BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Usiogope kufeli katika jambo fulani.


Wakati mwingine inapotokea umefeli katika jambo fulani basi hupaswi kuona kufeli huko kama ni njia ya kukata kwako tamaa au usione kama haiwezekani kwako kuweza kufanya vizuri katika jambo hilo ambalo umefeli.

Bali unachopaswa kujua ni kwamba watu wote ambao wamefanikiwa katika dunia hii wote hao kuna mambo fulani walifeli ndipo wakaja kufanya vizuri katika jambo fulani. Tafuta historia za watu hao ambao wamefanikiwa uone ni kwa namna gani watu  hao walifeli kabla ya kuwa ni watu wenye mafanikio, hapo ndipo utakapojua kuwa safari ya kuelekea mafanikio huanza na kufeli mara nyingi kabla ya kuja kufanikiwa.

Usiogope kufeli katika jambo fulani  kwa  sababu kufeli kupo pia ni njia ya kuelekea kwenye mafaniko kwa wale wanataka kweli kufanikiwa, hivyo unapaswa kuwa mvumilivu na kuona ni sehemu gani unazopaswa kuzirekebisha ambazo zitakuepusha kufeli mara kwa mara katika jambo fulani.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments