Unatakiwa kuwaepuka sana watu waliokata tamaa, watu ambao hawakazani kufanikiwa, watu wanaolalamika na kulaumu wengine. Watu wa aina hii watanyonya nguvu zako za mafanikio na hutaweza kupiga hatua yoyote ya maana.
Watu waliokata tamaa wao kila kitu kwao hawawezi kukifanikisha. Kazi yao kubwa wanakuwa ni watu wanaowakatisha tamaa wenzao wanaoweka juhudi za kuelekea kwenye mafanikio.
Najua umeshawahi kuwaona watu wa namna hii, kaa mbali nao. Huhitaji hata kushirikiana nao, maana ni watu ambao watakupotezea uelekeo wako, kwa sababu hao ni watu ambao wamekata tamaa mazima.
Zingatia sana, kushirikiana na watu wanaokutia moyo. Watu waliokata tamaa, achana nao na ni sumu kwako. Waepuke na wakimbie. Ukifanya hivyo utaweza kupiga hatua za kimafanikio kwa ukifanyacho.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.

0 Comments