Mafanikio yapo kama ladha ya chakula. Kama chakula unachokula kina ladha nzuri kwako, basi chakula hicho utaendelea kukila mara kwa mara mpaka utafanikiwa kukimaliza chote kabisa.
Na mafanikio yako yapo hivyo hivyo. Utaendela kufanikiwa kama unajua ladha ya kupenda kile unachokifanya. Kupenda kile unachokifanya hiyo ndio ladha ya mafanikio yako. Hakikisha ladha hiyo unaipenda na itakufanikisha.
Kosa kubwa la wengi ni kufanya mambo ambayo hawayapendi ilimradi tu wapate pesa. Huko ni sawa na kula chakula ambacho ladha yake huipendi, hautakila chote. Ishi kwa kufanya kile unachokipenda, na utafanikiwa.
Kwa mfano, kuvuta sigara leo au kunywa soda sana, unaweza ukaona ni kitu kizuri, lakini kwa baadae sana kitakupa shida wewe na kuwaathiri hata ambao hawakuhusika na hatua zako ulizochukua leo.
Mafanikio yanahusisha sana kufikiria matokeo ya mbele, na sio sasa tu. Ukiwa unafikiria matokeo ya mbele uhakika wa kufanikiwa upo, ila ukifikiria sasa peke yake utapotea na hautaweza kufanikiwa.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.

0 Comments