Jitahidi sana, usiwe mtu wa kuchanganyikiwa, kuweweseka au kupagawa kwa sababu ya mafanikio madogo unayoyapata. Mafanikio madogo unayoyapata yasikuvimbishe kichwa na kujiona wewe ndio kila kitu.
Wengi wanapokuwa na mafanikio madogo, basi kazi ya ulevi, uasherati na kutumia pesa hovyo ndipo inapoanzia hapo, kumbe wanasahau hawatakiwi kuchanganyikiwa na mafanikio madogo kwani si kitu.
Unachotakiwa kufanya ni kuweka misingi au mizizi imara kwenye mafanikio madogo na kuhakikisha hayapotei kwa namna yoyote na si kuanza kutapanya mafanikio hayo, hovyo hovyo na bila utaratibu.
Acha kujawa na kiburi, dharau na mafanikio kidogo ambayo hata hujui kesho kama yatakuwepo au hayatakuwepo kwako. Jichunge na mafanikio unayoyapata yasikupoteze. Acha mbwembe na mafanikio madogo.
Wako
rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu
kupitia WhatsApp.

0 Comments