BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mwangaza mpya katika maisha hutengenezwa hivi.


Ili uweze kuona mwangaza mpya katika maisha yako basi unatakiwa uweze kuongozwa na ubunifu ndani yako. Unapaswa kufanya kila kitu kwa kutanguliza ubunifu, kwani kufanya hivyo, kitu hicho ulichokiongezea ubunifu kitakuwa na thamani kwako na watu wengine ambao wanakuzunguka katika maisha yako.

Mwingine anaweza akahoji je ubunifu ni nini? Majibu ya swali hilo ni jepesi kabisa kwamba, ubunifu ni kufanya kitu kile kile ila kwa njia tofauti. Kwa mfano badala ya kusubiri wateja wako wakufuate hapo ulipo basi unapaswa kuanza kuwafuata walipo wateja hao ili kuwapelekea huduma na bidhaa. 

Huo ni kama mfano tu, ila kwenye kila sekta ambayo inakusu wewe ili uweze kuona mabadiliko na maendeleo makubwa basi unapaswa kutumia ubunifu ili uweze kujiongezea thamani katika jambo hilo. 

Wakati mwingine katika kufanya ubunifu wowote ule, kama itakulazimu kubadilisha ratiba zako za kiutendaji basi fanya hivyo kwa sababu wewe ndiye ujuaye ni kipi unachotaka. Ni muhimu  kila wakati kukumbuka maana ya ubunifu kisha kuishi katika ubunifu huo.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments