BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Siri pekee itakayokusaidia sana kufanikiwa.

Siri pekee itakayokusaidia sana kuweza kufanikiwa katika maisha na biashara ni kuwekeza muda wako mwingi katika kusoma vitu vitakavyokusaidia kukua katika eneo unalolifanyia kazi au unalotaka kufanyia kazi. 

Kama unataka kufanya biashara fulani basi wekeza muda wako katika kujifunza juu ya jambo hilo. Soma kwa undani juu ya biashara hizo ili kujua ni mbinu gani utatumia kuwakama wateja, pia ujifunze namna ambavyo utakabiliana na changamoto fulani hasa pale zitakapojitokeza katika eneo unalolifanyia kazi.

Pia ikumbukwe ni muhimu kusoma vitu vipya kila wakati kwa sababu, unaposoma vitu vipya kila wakati ni kwamba utaongeza uelewa wa kutosha katika kutenda jambo fulani. Pia kusoma hasaidia sana kuifanya akili yako kuwa vizuri zaidi katika jambo fulani. Soma vitu chanya kila siku kila inapowezekana.

Ikumbukwe tu, sina maana kwamba nina maana  ya kwamba unahitaji elimu ya darasani ikusaidia katika hili la hasha zipo elimu zingine ambazo ni elimu nje ya darasa ambazo wapo waandishi mbalimbali wamewekeza katika maarifa ambapo itakuhitaji wewe kuweza kujifunza kupitia maandiko yako, hivyo kazi ibaki kuwa kwako kuweza kusoma maandiko hayo.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments