BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Mtandao wa watu ni muhimu sana maishani mwako.

Ikiwa unataka kufanikiwa zaidi kwenye kile unachokifanya basi ni muhimu sana kuwa na mtandao mzuri wa watu. Bila kuwa mtandao mzuri wa watu ni kwamba utashindwa kufika viwango vya juu vya mafanikio yako. Utashindwa kufika viwango vya juu vya mafanikio yako kwa sababu kile unachokijua wewe utahisi kama kinatosha kumbe lah.

Ila unapokuwa na mtandao wa watu ni kwamba utajifunza mengi kupitia watu hao mwisho wa siku kile ambacho hukijui kwa ufasaha kupitia watu wengine utakwenda kukijua na kitakwenda kukuongezea thamani kwenye kile unachokifanya wakati mwingine kitakuongezea thamani kubwa  sana hata katika maisha yako kwa ujumla.

Hivyo ni muhimu sana katika maisha yako kuona ni kwa namna gani unaongeza mtandao wa watu mbalimbali kila wakati watakao kusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kufika viwango vya juu vya mafanikio yako, kwa kuwatumia watu hao kuweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo yatakuwa na faida kwako na jamii kwa ujumla.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments