BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Hivi ndivyo unavyoweza kuandika historia ya maisha yako.

Amua kuandika historia ya maisha yako kwa kuamua kufanya kile unachokipenda na tena kwa nguvu zako zote. Waonyeshe watu kwa vitendo kwa kile unachokifanya hubahatishi, bali unakijua ndani, pia unakijua kwa nje.

Kipi unachokifanya, basi kitu hicho amua kukifanya kwa ubora wa juu na kikupe matokeo makubwa unayoyataka. Hakikisha unachokifanya kinakufanikisha na kinakupa matokeo makubwa ambayo kila mtu atashangaa.

Andika historia kubwa ya maisha yako kwa hicho ukifanyacho. Kifanye mpaka watu wengine watakaotokea nyuma waje washangae ulifanyaje. Kuwa shujaa wa maisha yako mwenyewe kwa kufanya makubwa na ya kutisha.

Kama kuna watu walitengeneza historia ya maisha yao kwa jasho na damu, wewe leo, tengeneza historia ya maisha yako kwa kuamua kuchapa kazi, na kuchapa kazi mpaka kieleweke. Kazi yako ndio itaandika historia mpya ya maisha yako.

Wako rafiki katika mafanikio ; Imani Ngwangwalu

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

dirayamafanikio@gmail.com

BONYEZA HAPA http://wa.me/255687449428 ili kuwasiliana na Imani Ngwangwalu kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments