Kila siku unashauriwa na watalamu wa saikolojia kwamba unatakiwa kufanya tafakari (meditation). Tafakari (meditation) ambayo inakusu wewe binafsi hususani suala maisha yako kwa ujumla namna ambavyo utakuwa bora zaidi katika ngazi ya familia, kazi, mahusiano na uchumi kiujmla.
Pia watalamu hao wanasema kwamba kufanya tafakari (meditation) angalau kwa kila dakika 20 za kila siku huongeza uwezo wako binafsi wa kutatua changamoto zinazokukbali wewe binafsi.
Vile vile wanasema kwamba unapofanya tafakari (meditaion) unatakiwa kutafuta sehemu ambayo imetulia, pia sehemu hiyo pasiwepo na kelele zitakazokusaidia kuweza kutafakari vyema hasa yale yanayokuhusu.
Pia unapofanya tafakari (meditation), unapaswa kuwaza vyema jambo moja kwa umakini wa hali juu mpaka ulipatie majibu jambo hilo. Haupaswi kuwaza jambo fulani kisha kuishia njia, bali unapaswa kuwaza jambo fulani mpaka upate majibu sahihi ya jambo hilo.
Narudia tena umuhimu wa kufanya tafakari (meditation) husaidia sana kuweza kuimarisha uwezo wako wa kiakiri katika kutafuta majibu ya chanagamoto. Hivyo jifunze kufanya tafakari (mediation) kila siku ili uweze kujiimarisha katika uwezo wako wa kufikiri pia kutafuta majibu ya changamoto zinazokukabili.
Ndimi:
Afisa Mipango, Benson Chonya.
Bonyeza
hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail
BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.

0 Comments