BREAKING ARTICLES

6/recent/ticker-posts

Kanuni ya pesa unayotakiwa kuifahamu.

Kanuni muhimu ya pesa ambayo unatakiwa kuifahamu kila wakati ni kwamba “tumia pesa, kutengeneza pesa”. Mara nyingi watu wengi wamekuwa wakitumia pesa katika kutengeneza umaskini, wao kwenye kila pesa wanayoipata basi imekuwa ikitumika katika kufanya mambo ambayo hayana muendelezo wa kutengeneza pesa.

Kitu hicho kimechukua idadi kubwa ya watu, ambao watu hao vivywa vyao mara nyingi wamekuwa ni vinara wa kulalamika kwamba maisha ni magumu kila wakati. Na endapo watu hao hawatabadili namna ambavyo hutumia pesa yao basi ni watu hao wataendelea kulalamika maisha yao yote.

Ikiwa umechoshwa na hali ngumu ya maisha ambayo unaipitia hususani katika suala la pesa ni kwamba unatakiwa kuhakikisha kila wakati unatumia pesa kutengeneza, yaani kwenye kila pesa ambayo unaipata unatakiwa kutenga walau asilimia hata 20 kwa ajili ya uwekezaji na si kuitumia yote pasipo sababu za msingi, na hiyo ndiyo maana ya tumia pesa kutengeneza pesa.

Ndimi: Afisa Mipango, Benson Chonya.

Bonyeza hapa kuwasiliana nami kupitia E-mail

bensonchonya23@gmail.com

BONYEZA HAPA https://wa.me/255747030303 kuwasiliana nami kupitia WhatsApp.


Post a Comment

0 Comments